Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burna Boy ambwaga Diamond, Wizkid kwenye tuzo za BET

Bec718a3cdab6ee2 Burna Boy ambwaga Diamond, Wizkid kwenye tuzo za BET

Mon, 28 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Burna boy alikuwa anapigania tuzo hizo pamoja na mwimbaji staa wa Bongo Mtanzania Diamond Platinumz na Wizkid kutoka NigeriaBurna Boy alitajwa mshindi wa tuzo hizo mara tatu mfululizo mwaka 2019, 2020 na 2021Diamond aliwapongeza Watanzania licha ya kuendesha kampeni mtandaoni ya kutaka mwanamuziki huyo kuondolewa katika tuzo hizo

Mwanamuziki Damini Ebunoluwa Ogulu almaarufu Burna boy ndiye mshindi wa Tuzo za Muziki za BET.

Burna boy alikuwa anapigania tuzo hizo pamoja na wapinzani wake wakuu kimataifa akiwemo mwimbaji staa wa Bongo Mtanzania Diamond Platinumz na Wizkid kutoka Nigeria.

Katika hafla hiyo iliyoandaliwa Jumapili, Juni 28, nchini Marekani, Burna Boy alitajwa mshindi wa tuzo hizo mara tatu mfululizo mwaka 2019, 2020 na 2021.



Wengine waliokuwa katika kipengele hicho ni Aya Nakamura (Ufaransa),Emicida (Brazili), Headie One (Marekani) Young T & Bugsey (Marekani) na Youssoupha (Ufaransa).

Akizungumza baada ya hafla hiyo, msanii Diamond aliwapongeza Watanzania licha ya kuendesha kampeni mtandaoni ya kutaka mwanamuziki huyo kuondolewa katika tuzo hizo.

Diamond alisema kupitia tuzo hizo, alitambua namna Watanzania wana umoja, upendo na kuwashukuru kwa upendo waliomuonyesha.

"Kupitia tuzo hii nimeona ni kias gani watanzania tuna umoja, upendo na kuthamini vya kwetu...Nawashkuru sana kila mmoja wenu kwa Upendo mkubwa mlionionesha...Nifaraja kuona Dunia inapotaja nchi zenye Wanamuziki bora Tanzania inatajwa."

"Ni jambo la Kumshukuru Mungu....Na naamini wakati mwingine Tutaibeba...nitafarijika kesho na kesho kutwa msanii mwingine pia akiwa katika jambo la kuwakilisha Taifa tumpe nguvu kama mlionipa.... sis ni Swahili Nation sisi ni Taifa la Waswahili," aliandika muimbaji huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Tuzo za BET zilianza kutolewa mwaka 2001, zinazoandaliwa mahususi kwa ajili ya kusherehekea mafanikio ya kazi za Wamarekani weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji, michezo, zinatolewa usiku wa leo huko nchini Marekani.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke