Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burna Boy ageukia uigizaji

Burna Boy Has Postponed His Concert At FNB .jpeg Burna Boy

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkali wa Afrobeat kutoka nchini Nigeria, Burna Boy ameripotiwa kuingia kwenye tasnia ya filamu kama mtayarishaji mkuu katika filamu iitwayo ‘3 Cold Dishes’.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo Burna atataarisha filamu hiyo akishirikiana na kampuni ya filamu ya ‘Spaceship Films’, akiwa na meneja na mama yake mzazi #BoseOgulu.

Hii itakuwa filamu ya kwanza kwa Burna Boy baada ya kujitolea maisha yake kwenye muziki ambapo atashirikiana na baadhi ya mastaa wa filamu nchini humo akiwemo Asurf Oluseyi, mshindi wa Tuzo ya African Magic Viewer’s Choice (#AMVCA) 2016, Wale Ojo, Osas Ighodaro, Femi Jacobs, pamoja na waigizaji wengine kutoka Ivory Coast na Senegal.

BurnaBoy atakuwa ni mwanamuziki wa pili kujiingiza katika tasnia ya filamu kwa mwaka 2024 wa kwanza akiwa mwanadada Tiwa Savage na filamu yake iitwayo ‘Water and Garri’ ambayo ilianza kuoneshwa kwa mara ya kwanza Mei 10 kupitia Prime Video.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live