Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bruce Africa aungana na mashabiki wake kwenye shoo za mikoani

Bruce Africa 2299 Bruce Africa.

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: SnS

Bruce Africa yupo kanda ya Ziwa, ambako anaungana na mashabiki wake kwa lengo la kufurahia burudani za muziki wake. Hii ni kwa mara ya kwanza muimbaji huyo anawazungukia mashabiki wake waliopo nje ya Dar Es Salaam.

Kwenye mahojiano na SnS, muimbaji huyo amefunguka kuhusu safari yake ya kutembelea mashabiki wake waliopo nje ya miji mikubwa.

“Projekti hii niliipanga kuifanya baada ya mwezi wa Ramadhan, nimeanza na Kanda ya Ziwa, lengo kubwa ni kukutana na mashabiki na kupatana burudani kwa pamoja”. alisema

“Tangu nimeanza Ku-hit, sijawahi kuwa na utaratibu huu wa kufanya shoo mara kwa mara au kuzunguka ndani na nje ya Tanzania, nimeamua kuitumia fursa hiyo kujipima mimi kama mimi, hauwezi kukaa mjini ukasema wewe ni supastaa, ustaa wako ukoje?” Bruce aliongeza.

Bruce ameelezea kufurahishwa na mapenzi anayopewa naashabiki anaokutana nao, akidai anauona ukubwa wake baada ya kutoka Dar Es Salaam na kwenda kufanya shoo za vijijini, mahali ambako hakutarajia kupata mapokezi makubwa anayopewa na mashabiki wake hao, ambao anakutana nao kwa mara ya kwanza.

“Hii inaonyesha ukubwa wangu ukoje tofauti ningebaki mjini, nakutana na mashabiki wanaofurahia muziki ninaoufanya, wengine wanalia, wengine wananibeba juu. Ni upendo zaidi ya vile nilivyokuwa nafikiria”.

Bruce Africa amesema anaamini kuna nguvu kubwa kwa msanii kukutana na mashabiki zake, na kushirikiana nao kwa pamoja, inaongeza upendo. Mwenyezi Mungu anafungua milango na kutoa kibali, ninamshukuru Mungu kwa ajili ya hii.

Baada ya kumalizana na Kanda ya Ziwa, Bruce Africa anatarajia kuhamia Kanda nyingine, lengo likiwa ni kufurahia, na kuungana zaidi na mashabiki wake nje ya Dar Es Salaam.

Chanzo: SnS