Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking News: Msanii mkongwe Bi Sonia afariki Dunia

BI SONIA AFARIKI Breaking News: Msanii mkongwe Bi Sonia afariki Dunia

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji wa kitambo Farida Sabu ‘Bi Sonia’ amefariki dunia akiwa visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Tanzaniaweb.com imezipata kutoka kwa mtu wa karibu na familia, Bi Sonia amefariki leo Julai 21, 2022 ambapo kwa sasa taratibu za mazishi zinendelea kufanyika.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa, wasanii wenzake tayari wameanza kuungana kwa ajili ya kujua msiba utakuwa Zanzibar au jijini Dar.

Bi Sonia ambaye ni zao la Kundi la Kaole, amewahi kuonekana kwenye tamthiliya mbalimbali ikiwemo Tufani ambayo alicheza kama mama yake Johari. Tamthiliya nyingine ambazo Bi Sonia amecheza ni pamoja na Ndoano, Kapuni na Juakali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live