Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boxing Day yamtoa machozi Rihanna

669 Ksw1226 TZW

Wed, 27 Dec 2017 Chanzo: bongo5.com

Inauma sana unapo ondokewa na mtu wako wa karibu. Rihanna amejikuta katika kipindi kigumu baada ya furaha ya kusherehekea sikukuu ya Christmas Jumanne hii kugeuka huzuni.

Tavon Alleyne akiwa na Rihanna wakisherehekea sikukuu ya Christmas kabla ya kupigwa risasi

Msanii huyo amepatwa na msiba wa ndugu yake wa kiume [binamu yake] Tavon Kaiseen Alleyne, 29, ambaye amefariki dunia Jana baada ya kupigwa risasi katika maeneo ya St Michaels, Barbudos.

Tukio hilo limetokea baada ya kupita saa moja walipoachana ambapo Rihanna na Tavon walikuwa wakisherehekea pamoja sikukuu hiyo.

Riri ameonyesha kuumizwa sana na tukio hilo, kupitia mtandao wake wa Instagram ameandika ujumbe unaosomeka, “RIP cousin… can’t believe it was just last night that I held you in my arms! never thought that would be the last time I felt the warmth in your body!!! Love you always man!

Chanzo: bongo5.com