Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Bosi ajishusha kwa familia zilizoathiriwa na Mitandao

Mark Zuckerberg.jpeg Mark Zuckerberg

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Meta, Mark Zuckerberg ameomba radhi kwa familia zinazodai watoto wao waliathiriwa na maudhui ya mitandao ya kijamii.

Zuckerberg ambaye anamiliki WhatsApp Instagram na Facebook amesema hayo katika mkutano wa Bunge nchini Marekani ambapo ulihusisha viongozi wa Tiktok, Snapchat, X(Twitter) na Discord.

Hata hivyo Wabunge walitaka kujua hatua zinazochukuliwa kuwalinda watoto mitandaoni, ambapo pia walizungumza na baadhi ya familia ambazo zilisema watoto wao walijidhuru na wengine kujiua kutokana na maudhui ya mitandao ya kijamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live