Mwajiri kutoka Nigeria, aliyetambulika kwa jina la Oga Yenne, amelalamika mtandaoni baada ya kuwanasa wafanyakazi wake wakirushana roho.
Bosi huyo alisema amechoka nao. Kwa hisani ya Picha: Oga Yenne Chanzo: UGC Yenne aliwanasa kwenye kamera bila wao kujua na kushiriki kipande hicho kwenye Facebook, akilalamika jinsi alivyochoshwa na mapenzi yao ya ofisini.
Yene alisema alidhani watafunga ndoa 2023 lakini alikatishwa tamaa. Aliandika kwenye Facebook:
“Kwa kweli nilitarajia kuhudhuria ndoa ya wafanyakazi wangu hawa wawili mwaka huu. Lakini waliniangusha. Naomba walibebe hili penzi lao la ofisini hadi mwaka ujao."
Mfanyakazi wa kike alionekana kuwa kwenye simu katika kipnde hicho huku mwenzake wa kiume akiwa amepumzisha kichwa chake kwenye mapaja yake.