Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Bosi BBC ateuliwa kuwa bosi CNN

Sir Mark Thompson Sir Mark Thompson.

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la habari la BBC na Gazeti la New York Times, Sir Mark Thompson ameteuliwa kuliongoza Shirika la habari la CNN baada ya mfululizo wa migogoro na kushuka kibiashara kwa shirika hilo la habari.

Sir Mark anachukua nafasi ya Chris Licht aliyehangaika kuliweka sawa Shirika hilo la habari kwa miezi 13 akiwa kama Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu.

CNN imepitia misukosuko kadhaa iliyosababisha kufukuzwa kazi kwa waandishi maarufu kama Chris Cuomo na Don Lemon na kufungwa kwa huduma ya CNN+ ambayo ilidumu kwa mwezi mmoja.

Sir Mark anakabiliwa na changamoto ya kuiongoza CNN wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Marekani mwaka 2024.

Changamoto hiyo itagongana na kusimamia utangazaji wa habari kuhusu mashtaka ya kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live