Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#Boomplay:Rayvanny na Zuch waongoza orodha kwa kusikilizwa Tanzania

JJJJJJ9999 660x400 #Boomplay:Rayvanny na Zuch waongoza orodha kwa kusikilizwa Tanzania

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

App namba moja kwa huduma ya muziki Barani Afrika, Boomplay imemtaja msanii Rayvanny kuwa ndiyo mwanamuziki wa kiume aliyesikilizwa zaidi Tanzania huku Zuchu akiwa ndiyo mwanamuziki wa kike aliyesikilizwa zaidi Tanzania. Hii ni kwa mujibu wa taarifa na takwimu rasmi za muziki kwa mwaka 2020.

Taarifa hiyo iliyowekwa kwenye ripoti maalumu kuhusu muziki imeegemea zaidi kwenye data kutoka katika app hiyo ya muziki ambayo kwa mwezi ina wastani wa watumiaji milioni 50 ulimwenguni kote. Boomplay inajivunia kuwa na aina tofauti za nyimbo ambazo idadi yake ni zaidi ya milioni 44, ambazo zinapatikana kwenye iOS, Android na web huku ikiwa na jumla ya wasanii milioni 3.4 duniani kote.

Kwa kuanza na wasanii wa kiume watatu wa kwanza waliosikilizwa zaidi nchini Tanzania, Rayvanny anashika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Diamond Platnumz katika nafasi ya pili huku Harmonize akishika nafasi ya tatu.

Wasanii wa kike watatu wa kwanza nchini Tanzania waliosikilizwa zaidi ni Zuchu akishika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Nandy katika nafasi ya pili huku Maua Sama akishika nafasi ya tatu. Zuchu pia ametawala katika kipengele cha Nyimbo tatu kutoka kwa wasanii wa Tanzania zilizoongoza kusikilizwa ambazo ni Wana, Raha na Kwaru, zote hizo kutoka kwenye albamu ya Zuchu ‘I am Zuchu’.

Burna Boy ameongoza orodha ya wasanii wa kiume waliosikilizwa zaidi katika nchi zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara huku Simi akifanya hivyo kwa upande wa wasanii wa kike.

Boomplay pia imetoa taarifa za mwenendo na tabia za namna muziki unavyosikilizwa Tanzania. Katika taarifa hiyo maalumu, Bongo Flava imeongoza kwa kusikilizwa ikifuatiwa na nyimbo za Injili (Gospel) huku Afropop & Afrofusion ikishika namba tatu.

HARMONIZE KAFUNGUKA WANAOSEMA HAJUI KUONGEA KINGEREZA ‘NIMEISHIA FORM 3/USHAMBA WIMBO BORA KWASASA’

Chanzo: millardayo.com