Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bongo Fleva inaenda mbali, Diamond anaipushi sana – Shilole

822 Srgbfgy

Sat, 30 Dec 2017 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa Bongo Fleva, Shilole amedai kuwa muziki wa Bongo Fleva kwa sasa unakua kwa kasi duniani na kuufanya muziki huo kubadilisha maisha ya Wasanii huku akimtaja Diamond Platnumz kama moja ya wasanii wanaopambana kukuza muziki huo.

Shilole

Shilole amesema kuwa kitendo cha Diamond Platnumz kufanya kolabo na Wasanii wakubwa wa nje ya bara la Afrika kimefanya muziki wa Bongo Fleva kukua kwa kasi.

“Bongo Fleva inaenda mbali sana, hususani! tuseme ukweli Diamond anaipushi sana Bongo Fleva yetu, sikutegemea kama  Diamond siku moja atafanya ngoma na Rick Ross sijui na akina Ne-Yo nilikuwa nikiona tuu tutafika huku? lakini tumeanza kujaribu na tunafika..Natamani na mimi siku moja nifanye kazi na Nicki Minaj.“amesema Shilole kwenye mahojiano yake na BBC Swahili.

Shilole ambaye yupo nchini Uingereza alikoenda kutumbuiza kwenye show maalumu amesema kuwa show za nje ya nchi siku hizi zinalipa tofauti na zamani.

 

Chanzo: bongo5.com