Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Filamu Kenya yaifungia filamu ya ‘Rafiki’

7163 WhatsApp Image 2017 06 19 At 8.36.02 AM E1497857700502 400x242 TZW

Sun, 29 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Bodi la Filamu la Kenya (KFCB) imeipiga marufuku filamu ya Rafiki ambayo ndani yake inagusia mapenzi ya jinsia moja.



Bodi hiyo imepiga marufuku filamu hiyo kuonyeshwa hadharani au kutangazwa kwenye televisheni na kusambazwa, ikisema maudhui ya filamu hiyo inayoonesha mapenzi ya jinsia moja kati ya wanawake wawili, inakiuka sheria za Kenya.

Muongozaji na muandishi wa filamu ya Rafiki, Wanuri Kahiu, kupitia mtandao wa Twitter amethibitisha kufungiwa kwa filamu hiyo.

“I am incredibly sorry to announce that our film RAFIKI has been banned in Kenya. We believe adult Kenyans are mature and discerning enough to watch local content but their right has been denied. #Cannes2018 #AKenyanFirst,” ameandika Wanuri.

Chanzo: bongo5.com