Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Blac Chyna anayotengeneza mabilioni kupitia mtandao wa OnlyFans

Black Chyn Nmb.jpeg Blac Chyna

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamitandao wa Marekani, Blac Chyna kwa sasa ndiye kinara wa kutengeneza pesa kwenye mtandao wa OnlyFans, ametajwa kuingiza kiasi cha ($20 million) zaidi ya TSh. Bilioni 46 kila mwezi kwa mwaka 2021.

Chyna hutoza kiasi cha ($19.99) takribani TSh. Elfu 46 kwa mwezi kutazama maudhui yake ya picha na video kwenye Jukwaa hilo maarufu.

Chyna mwenye umri wa miaka 34 na watoto wawili, ametengeneza kiasi cha ($240 million) zaidi ya TSh. Bilioni 560 kwa mwaka 2021 kupitia akaunti yake ya OnlyFans.

Mbali na Blac Chyna, nafasi ya pili imeenda kwa mwigizaji Bella Thorne ambaye alitengeneza ($11 million) zaidi ya TSh. Bilioni 25 kwa mwezi mwaka 2021.

Cardi yupo namba 3 akiingiza ($9.34 million) zaidi ya TSh. Bilioni 22 kwa mwezi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live