Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti ya Snoop Dogg Cori Broadus apata kiharusi

Binti Ya Snoop Dogg Cori Broadus Apata Kiharusi Binti ya Snoop Dogg Cori Broadus apata kiharusi

Sat, 20 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Cori Broadus, bintiye rapa Snoop Dogg, amesema aliangua kilio wakati madaktari walipomwambia kuwa alikuwa na "kiharusi " akiwa na umri wa miaka 24.

Broadus alisambaza habari hiyo pamoja na picha zake kwa wafuasi wake 657,000 katika mtandao waInstagram siku ya Alhamisi akiwa amelazwa kwenye kitanda cha hospitali,

Alitoa maoni: "Nilipata kiharusi kikali mapema leo. Nilianza kuangua kilio waliponiambia.

"Nina umri wa miaka 24 tu. Nilifanya nini katika siku zangu zilizopita ili kustahili haya yote?"

Madaktari wakati mwingine hutaja kiharusi kama mshtuko wa moyo kwa ubongo.

Inatokea wakati damu inaposhindwa kufika katika ubongo.

Akijibu marafiki waliomtumia salamu za heri kwenye Instagram, Broadus alichapisha: "Nawapenda nawapenda."

Mwanamuziki na mjasiriamali Snoop Dogg, ambaye jina lake halisi ni Calvin Cordozar Broadus Jr, pia ana wana wawili, Corde na Cordell, na mkewe Shante.

Rapa huyo alijipatia umaarufu mkubwa kufuatia kutolewa kwa albamu yake ya kwanza ya mwaka 1993, Doggystyle - iliyotayarishwa na Dr Dre.

Chanzo: Bbc