Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti pekee wa Presley, mwanamuziki Lisa Marie Presley afariki dunia

Binti Pekee Wa Presley, Mwanamuziki Lisa Marie Presley Afariki Dunia Binti pekee wa Presley, mwanamuziki Lisa Marie Presley afariki dunia

Fri, 13 Jan 2023 Chanzo: Bbc

Lisa Marie Presley, mtoto pekee wa nguli wa muziki wa rock'n'roll Elvis, amefariki akiwa na umri wa miaka 54, mama yake amesema.

"Ni kwa moyo mzito kwamba lazima nishiriki habari mbaya kwamba binti yangu mrembo Lisa Marie ametuacha," Priscilla Presley alisema.

Lisa Marie, pia mwimbaji, alikimbizwa hospitalini mapema Alhamisi. Ripoti za vyombo vya habari zinasema alipatwa na mshtuko wa moyo.

Alikutwa akiwa hajifahamu nyumbani kwake huko Calabasas, California, vyanzo viliiambia TMZ ya Marekani.

"Alikuwa mwanamke mwenye mapenzi, nguvu na upendo zaidi ambaye nimewahi kushuhudia," Priscilla Presley alisema katika taarifa yake. "Tunaomba faragha tunapojaribu kukabiliana na hii kubwa,". Mama yake hakutoa maelezo yoyote kuhusu chanzo cha kifo.

Akizaliwa mwaka 1968, Lisa Marie aliendelea kufuata nyayo za baba yake na akajiingiza kwenye kazi ya muziki. Nyota huyo alitoa albamu tatu, huku albamu yake ya kwanza ya mwaka wa 2003 ikiuza mamia ya maelfu ya nakala na kupokelewa vyema kwa ujumla.

Nyota huyo pia alijulikana sana kwa kuwa na msururu wa mahusiano na watu maarufu akiwemo nguli wa pop Michael Jackson, mwigizaji Nicholas Cage na wanamuziki Danny Keough na Michael Lockwood.

Alikuwa na watoto watatu, akiwemo mwigizaji Roxy Keough. Kijana wake, Benjamin Keough, alijiua mnamo 2020.

Presley alionekana hadharani kwa mara ya mwisho Jumanne usiku kwenye tuzo za Golden Globes huko Beverley Hills.

Chanzo: Bbc