Wanadamu wanatumia lugha ya ishara inayofanana na wanyama kundi la nyani, sokwe,tumbiri na kadhalika.
Hilo ndilo hitimisho la utafiti unaotegemea video ambapo watu waliojitolea walitafsiri ishara za nyani.
Utafiti huo ulifanywa na watafiti katika Chuo Kikuu cha St Andrews.
Unapendekeza kwamba babu wa mwisho tuliyeshirikishana na sokwe alitumia ishara zinazofanana, na kwamba huo unaweza kuwa "chimbuko la" lugha yetu.
Matokeo ya utafiti yamechapishwa katika jarida la kisayansi la PLOS Biology.
Mtafiti mkuu, Dk Kirsty Graham kutoka Chuo Kikuu cha St Andrews alieleza: "Tunajua kwamba sokwe na nyani wale wanyama wakubwa - wana mwingiliano wa takriban 95% kwa ishara wanazotumia kuwasiliana.
"Kwa hivyo tayari tulikuwa tunashuku kwamba hii ilikuwa lugha ya ishara ilioshirikishwa na babu yetu wa mwisho..."
Utafiti huu ulikuwa sehemu ya dhamira inayoendelea ya kisayansi kuelewa chimbuko asili la lugha ya ishara kwa kufanya utafiti makini wa mawasiliano katika binamu zetu wa karibu kundi la nyani.