Rapa Bilnass amesema katika maamuzi ya maana aliyowahi kufanya katika maisha yake ni kumuoa Nandy.
Licha ya maneno ya wengi kuwaelekea wanadoa hao lakini anaona kwamba hajakosea kumuoa Nandy.
Bilnass anasema
"Nilifanya maamuzi sahihi kumuoa Nandy, nimemuoa mtu sahihi nimemuoa mtu ambaye niko proud nae ata ikitokea leo hii labda ningekuwa nimezaliwa tena alafu nifikilie kuoa, ningemuoa yeye tu nisingeenda sehemu nyingine"
"Huko nyuma kuna mambo yalitokea kila mtu anajua sitaki kuyazungumzia, tulifikia hatua tukaachana lakini upendo kila mara unaturudisha pamoja, changamoto tulizopitia zilikuwa ni namna ya kujifunza tuone ni kwa kiasi gani kila mmoja anamhitaji mwezie kwasababu mnapoachana unapokuwa na mahusiano mengine unagundua thamani ya uliyemuacha alikuwa ni bora zaidi"