Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Billnass asimulia alijifunza kwa marehemu Godzilla

BILLNASS NA GODZILLA Billnass asimulia alijifunza kwa marehemu Godzilla

Sat, 11 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Billnass amefunguka alichojifunza katika maisha ya marehemu Rapa Godzilla ambaye alikuwa naye karibu katika maisha yake ya muziki na kujifunza vingi huku akishuhudia mapito ya wasanii wengine ambayo yamemfanya agundue kazi ya muziki walioichagua wasanii ni ngumu sana.

“Mara zote ambacho najifunza kupitia hiyo (maisha ya Godzilla) na baadhi ya vitu ambavyo nimeviona, kwanza kazi ya sanaa ni kazi ngumu sana tumechagua, ina side effect nyingi sana.

"Unajua mimi kwa mfano ningekuwa nafanya kazi ofisini siku nikifukuzwa kazi atajua mke wangu, watoto, familia yangu pamoja na watu wanaonihusu, watajua sasa hivi Baba hana kazi na mambo sio mazuri na tutaendana nayo hivyo,” Rapa huyo alimwambia Sallam Jabir kupitia YahStoneTown.

“Lakini kimuziki ikifikia wakati sifanyi vizuri Tanzania nzima itakuwa inajua sasa hivi Billnass hafanyi vizuri. Kwa hiyo maneno ya watu na vitu watu watakuwa wanazungumza nikivipokea vinaweza kunipeleka sehemu mbaya, na kwa bahati mbaya kwenye mabaya watu watahusisha nafasi yako, jina lako, wanaweza kusema wewe pamoja na jina lako haustahili kukosa hicho kitu kabisa.

Kwa hiyo kwenye matumizi watasema wewe unastahili hili au unapaswa kunywa kunywaji hichi, lakini kwenye kuingiza ni tofauti, kwa wenzetu ni sawa kwa sababu watu wanalipwa kutokana na ukubwa wa majina yao.”

Aliongeza, “Kwa hiyo mfumo wetu unatengeneza maswali mengi, mtu anaweza kutokea wewe Billnass hautakiwi kukaa kwenye nyumba hii, haijakaa kisanii lakini hivyo vitu vyote vinahitaji hela ambayo hela hiyo mimi ni ngumu kuipata kwenye muziki huu. Kwa hiyo huu mfumo unatengeneza masikini wengi sana, tunakuwa na majina makubwa lakini hatupati hela.”

Hata hivyo, alisema sio wasanii wote wanaweza kufanya biashara na muziki, wasanii wengi wanafanya muziki kwa ubora wa hali ya juu wakiamini ndio njia yao pekee ya kutengeneza pesa.

Amesema Godzilla alikuwa ni msanii na producer wa kutengeneza beat, lakini pia alikuwa anafanya vitu vingine na vilikuwa vinamtosha kuyafanya maisha yake kuwa bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live