Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Billnass apewa muongozo BASATA baada ya kufungiwa miezi 3

Billnasa Apewa Muongozo BASATA Baada Ya Kufungiwa Miezi 3 Billnass apewa muongozo BASATA baada ya kufungiwa miezi 3

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kufungiwa miezi mitatu kwa kutojihusisha na kazi za sanaa na ‘faini’ ya milioni tatu, staa wa Bongo Fleva, Billnass naye amefika Baraza la Sanaa Taifa BASATA na kupatiwa muongozo wa maadili katika kazi za sanaa.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa BASATA wame-share picha ya Nenga akikabidhiwa muongozo huo siku ya jana na Katibu Mtendaji BASATA, Dkt Kedmon Mapana.

Billnass alifungiwa kutojihusisha na kazi za sanaa Novemba 7 kutokana na kushirikishwa kwenye wimbo wa ‘Ameyatimba’ wa Whozu, ambao maudhui ya video yake yanatajwa kukiuka kanuni za maadili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live