Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Billnass: Wimbo wangu na Diamond utasimamisha nchi

Billnass Ft Diamond Platnumz Mikausho Mikali Billnass na Diamond.

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapper maarufu Bongo, Billnass kutokea nchini Tanzania ameweka wazi ujio wa nyimbo aliyoifanya na Diamond Platnumz ikiwa ni baada ya wiki moja tu baada ya kuachia nyimbo yake mpya aliyofanya na staa kutoka WCB Mbosso.

Billnass amefunguka kuwa hivi karibuni ataachia kolabo yake na Diamond Platnumz na itakuwa kazi kali na kubwa kuwahi kutokea maishani mwake.

Billnass amesema;"Katika nyimbo zangu zote nyimbo niliyofanya na Diamond sijui hata nisemeje ila ni history na ndio nyimbo kali na nikiichia mji utatifuka. Alianza kuiachia mapozi kwa sababu ndo ilirekodiwa kwanza halafu baadaye tutaachia hiyo yangu.

"Wimbo wangu na Diamond ni wimbo mkubwa na mkali sana. Naiamini muda wowote nikiachia najua panatimka panatifuka na tunapindua juu chini," amesema Billnass.

Kwa unavomjua Billnass unahisi kolabo na Diamond itakuwaj?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: