Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Billnas afunguka kuhusu mtoto wa Mobetto na Diamond

Nenga A0000 Billnas afunguka kuhusu mtoto wa Mobetto na Diamond

Sat, 5 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Staa wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Billnas amesema anasikitishwa na taarifa za mitandaoni zinazodai kwamba Dylan mtoto wa Hamissa Mobetto ni mtoto wake.

Billnas amesema hajawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Hamissa Mobetto, ingawa kuna kipindi wamewahi kuwa marafiki lakini wakati huo tayari Hamissa alikuwa amemzaa mtoto huyo na jamii nzima inatambua kama mtoto ni wa Diamond Platnumz.

"Kimsingi mimi sifanani na huyo mtoto kabisa, ila unajua kitu kikishasemwa sana na ukikiamini unaanza kuona kama ni kweli, watu wanachukua picha ambazo zina mfanano kiasi wanaziambatanisha kisha wanaanza kutufananisha.

"Inaniumiza kwasababu najua haimfurahishi mama yake, na siyo mama yake tu, mwanamke yeyote hawezi kufurahishwa na kitendo cha mtoto wake kufananishwa na mwanaume ambaye hajawahi kuwa naye kwenye mahusiano," amesema Billnas.

Aidha Billnas ameongeza kuwa haimuumizi mke wake Nandy kwasababu anaujua ukweli toka mwanzo, amesisitiza kuwa mtoto ni wa Diamond Platnumz. Kuhusu ukaribu wake na Diamond baada ya tuhuma hizo.

Billnas amesema yeye na Diamond hawana shida, ni marafiki wazuri wanawasiliana na hata kipindi cha mwezi wa Ramadhani mwaka huu alienda kufturu siku moja nyumbani kwa Diamond Platnumz ambapo alialikwa na Diamond mwenyewe.

Chanzo: Mwanaspoti