Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bill Nass ajibu ngoma yake ‘Tagi Ubavu’ kukopi beat ya Bongo Bahati Mbaya

3853 Adadadad TZW

Thu, 1 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki Bongo, Bill Nass amefunguka madai ya kuwa ngoma yake mpya ‘Tagi Ubavu’ imekopi beat kutoka kwenye ngoma ya Young Dee ‘Bongo Bahati Mbaya’.



Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa si kweli kwamba ngoma hiyo imefanana na Bongo Bahati Mbaya ila ni aina ya muziki kama ilivyo trap ambao mara nyingi beat zake huwa kama zimefanana.

“Sio kweli, hiyo ni aina fulani ya muziki kama trap beat, unaweza kumuuliza producer Mr. T ina muda gani kazi yangu, lakini ni tofauti kabisa kuanzia flow, melody na kila kitu ni tofauti,” amesema.

“Kuna muendano tu katika aina ya mdundo kwa mbali na hivyo ni vitu ambavyo vinafanyika kwenye muziki, hata sasa hivi naweza kupenda muziki wa Dkt. Remy Ongala tukafanya muziki,” amesema.

Ngoma ya Tagi Ubavu inakuwa ngoma ya nne kwa Bill Nass kufanya kwa Mr. T Touch baada ya hit kama Chafu Pozi, Mazoea na Ligi Ndogo. Bill amesema sababu ya kufanya kazi nyingi na producer huyo ni kama ni mtu ambaye anampatia sana, pia ana uwezo mkubwa.

Chanzo: bongo5.com