Tajiri wa India, Ratan Tata amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86, imesema Tata Group, muungano wa makampuni alioongoza kwa zaidi ya miongo miwili.
Tata alikuwa mmoja wa viongozi wa biashara wanaotambulika kimataifa nchini India.
Kundi la Tata ni mojawapo ya makampuni makubwa zaidi ya India, yenye mapato ya kila mwaka ya zaidi ya $100bn (£76.5bn).
Katika taarifa ya kutangaza kifo cha Tata, mwenyekiti wa sasa alimtaja kama "kiongozi wa kipekee".
Natarajan Chandrasekaran aliongeza: "Kwa niaba ya familia nzima ya Tata, ninatuma salamu zetu za rambirambi kwa wapendwa wake.
"Alichoanzisha kitaendelea kututia moyo tunapojitahidi kuzingatia kanuni alizotetea kwa dhati."
Waziri wa Biashara wa Uingereza Jonathan Reynolds alisema kwa heshima kwamba Tata alikuwa "nguzo muhimu katika ulimwengu wa biashara" ambaye "alichukua jukumu kubwa katika kuunda tasnia ya biashara Uingereza".