Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bila woga! Baba Levo aanika mapungufu ya Diamond

Baba Levo Na Diamond Bila woga! Baba Levo aanika mapungufu ya Diamond

Fri, 13 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chawa na mtangazaji wa Wasafi FM, Baba Levo, ameanika mapungufu ya bosi wake, Diamond Platnumz kwa kusema, jamaa sio mtu wa kupokeapokea simu.

Baba Levo ameyasema hayo kupitia luninga moja ya mtandaoni ambapo mtangazaji wa luninga hiyo, alitaka kujua mapungufu ya staa huyo ambaye kila uchwao amekuwa akimsifia kwa mazuri yake.

"Hakuna mwanadamu asiye na mapungufu, Diamond anayo yake lakini yanazibwa na yale mazuri mengi anayoyafanya. Mfano, tunapoongelea mapungufu, kuna wakati mimi nilifanya kazi sana lakini sikuongezwa mshahara wakaongezwa wenzangu.

"Lakini pia simu, unaweza kumpigia sana asipokee lakini hilo ni jambo la kawaida maana akiwa na jambo muhimu atakucheki na mtafanya," alisema Baba Levo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live