Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bifu la Tylor na Kanye kurudi tena!

Bifu La Tylor Na Kanye Kurudi Tena! Bifu la Tylor na Kanye kurudi tena!

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huwenda Bifu La Taylor Swift Na Kanye West Likarudi Tena, Kwani Mwanamuziki TaylorSwift Ameliambia Jarida La "TIME" Kwamba Alienda Nchi Nyingine Baada Ya 'Kim Kardashian" Kuvujisha Mazungumzo Yake Ya Siri Na #KanyeWest

Kama Unakumbuka Kanye kupitia wimbo wake uitwao “Famous” uliotoka mwaka 2016 Ali-Rap “made that bitch famous,”Yani Akimaanisha Kwamba Alimfanya Taylor Swift Apate Umaarufu, Jambo Ambalo Lilipelekea Swift Kulalamika kuwa amedhalilishwa. Kanye alidai kuwa mstari huo uliruhusiwa kuwepo na Swift kabla ya wimbo kutoka. Hivyo Mgogoro Huo Ulifufua Bifu Lao La 2009

Hata hivyo Aliyekuwa mke wa Kanye West, Kim Kardashian alivujisha video Kama Uthibitisho ikimuonyesha Kanye West akiwa anaongea na Taylor Swift kupitia simu na walikuwa wanajadiliana kuhusu wimbo huo na mwisho Taylor Swift alikubali wimbo huo utoke. Lakini wakati Kanye anaomba ruhusa ya Taylor Swift kuitoa ngoma hiyo hakumuambia Taylor Swift Kuhusu maneno hayo Ya Matusi.

Bifu La Kanye Na Taylor Lilianza Mwaka 2009 Katika Tuzo Za MTV ambapo Taylor Swift alitangazwa mshindi wa nomination ya “Best Female Music Video” kupitia wimbo wake wa “You Belong With Me”.

Katika hali ya kushangaza Kanye alipanda kwa stage na kumnyang’anya mic Taylor kisha akasema;

“Yo, Taylor, I'm really happy for you, I'mma let you finish. But Beyoncé had one of the best videos of all time! One of the best videos of all time!”

Akimaanisha kuwa Taylor hakuwa mshindi sahihi wa tuzo hiyo bali #Beyonce ndiye alipaswa kuchukua tuzo hio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live