Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bifu la Kim na Taylor Swift laanza upya

Taylor Swift And Kim Kardashian Friends Bifu la Kim na Taylor Swift laanza upya

Sat, 20 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Album mpya ya mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Taylor Swift iitwayo ‘The Tortured Poets Departmen’ imeripotiwa kuwa nyimbo moja ambayo imemuongelea mfanyabiashara #KimKardashian.

Kwa mujibu wa tmz imeeleza kuwa album hiyo inayotarajiwa kuachiwa siku ya leo wimbo uitwao ‘thanK you aIMee’ umedaiwa kuwa ni dongo kwenda kwa Kim kutokana na herufi kubwa zilizokuwepo kwenye jina la wimbo huo zinazotajwa kuwa jina la #Kim (KK).

Endapo ngoma hiyo itakuwa ni dongo kwenda kwa Kim basi #Swift atakuwa hajamaliza ugomvi wake na mfanyabiashara huyo.

Ikumbukwe kuwa bifu la Kim na Swift lilianza mwaka 2016 baada ya aliyekuwa mume wa #Kim, #kanyewest est kutoa wimbo wa ‘#Famous’ uliokuwa ukieleza kuwa Kanye ndiyo amefanya Taylor kuwa maarufu huku ikidaiwa kuwa Kim alihusika katika uandishi wa ngoma hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live