Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bifu la Chris Brown, Quavo lapamba moto

Quavo X Brizzy Bifu la Chris Brown, Quavo lapamba moto

Sun, 21 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ‘rapa’ Quavo kumjibu mwanamuziki Chris Brown kupitia ngoma yake ya ‘Tender’ ambayo mashairi yake yanamtuhumu Brown kuwa alikuwa akimdhalilisha mpenzi wake wa zamani, na sasa Chris amemjibu Quavo kupitia ngoma yake ya ‘Weakest Link’.

Kupitia ngoma hiyo Chris amemchana Quavo kupitia mashairi yake yaliyokuwa yakieleza kuwa ulilala na ex wangu lakini hata mimi pia nililala na ex wako wakati bado upo naye, na kwa mujibu wa baadhi ya vyombo vya habari vinadai kuwa ex wa Quavo aliyelala na Brown ni Saweetie.

Quavo na#Chris Brown wapo katika bifu toka mwaka 2017 baada ya Quavo kudaiwa kutoka kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wa #ChrisBrown Karrueche Tran.

Aidha wasanii wa hip-hop nchini Marekani wapo moto kurushiana madongo kupitia ngoma wanazoziachia ambapo siku mbili zilizopita mwanamuziki #Drake ameposti ngoma yake mpya ambayo ametumia AI kuingiza sauti ya Snoop Dogg na Marehemu #Tupac ngoma hiyo ikidaiwa kuwa amemjibu Kendrick #Lamar huku Drake akimtaka Lamar kujibu ngoma hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live