Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bifu kubwa zilizowahi kutoa kati ya mastaa wa muziki na AKA

Aka Dead Mds Bifu kubwa zilizowahi kutoa kati ya mastaa wa muziki na AKA

Tue, 14 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni kawaida kwa mastaa kuwa kwenye misuguano ya hapa na pale wao kwa wao hasa linapokuja suala la mmoja kutaka kujiona ni zaidi ya mwingine. Hadi rapa AKA anaondoka duniani, hizi ni bifu zake kubwa 5 ambazo amewahi kujihusisha nazo.

1. CASPPER NYOVEST, bifu lao lilikuwa linagusa muongo mmoja sasa tangu waanze kupishana mwaka 2013. Kwa mwaka 2013 hadi 2015 wawili hao walijikuta wapo kwenye mchuano mkali, head to jead kwenye tuzo hadi kwenye media (Tv & Radio) Chart show, hili lilisababisha wawili hawa kutupiana maneno makali mitandaoni na kila mmoka akiweka wazi kutompenda mwenzie, kwenye moja ya podcast interview, Caspper Aliwahi kiri kuwa AKA anaogopwa na wasanii wengi sana kwenye game ila yeye kajitolea kumwambia bado ni kijana mdogo “Small Boy”.

Caspper alidai alimtaka mara kadhaa kumaliza tofauti zao ila AKA akakataa. October 2022 wawili hao walionekana kuzika tofauti zao kabla ya Caspper kukiamsha tena kwa kuedit picha ya AKA akiwa kashikilia kinywaji chake na kumtangaza kama Balozi wa kinywaji hicho.

2. BURNA BOY, ni baada ya mwaka 2019 kutangaza kutokanyaga ardhi ya Afrika Kusini kutokana na raia wa nchi hiyo kuua wageni (Xenophobia) huku akimchana AKA kama miongoni mwa watu wenye uwezo wa kukemea hayo ila kwake ni kama anafurahia. Mwaka 2022 wawili hao ambao tayari wana kolabo 3, walimaliza tofauti zao.

3. BLACK COFFEE, Ni baada ya Dj huyo mwenye tuzo ya Grammy (2022) kumchapa kofi la uso meneja wa AKA aitwaye Tshiamo Letswene. 2016 kwenye moja ya Tamasha huko Limpopo, AKA alikuwa anajiandaa kuperform lakini bila kupeana taarifa na Dj Black Coffee, Letswene alipanda jukwaani ghafla na kutaka msanii wake apande, akaambulia makofi.

4. ANATII, 2015 alimtengenezea hit AKA inaoitwa “The Saga” miezi michache mbele, AKA alitoa Disstrack inayoitwa “Composure” akimchana Anatii kwa kutaka kulipwa milioni 10.4 tsh kwenye kila beat ambayo alimtengenezea kisa tu The Saga kuwa kubwa.

5. Da L.E.S, licha ya kuwa marafiki wa kushibana waliishia kwenye uadui mkubwa bila kuwepo kwa sababu za msingi, Bifu hilo lilioneka kumalizika baada ya AKA kumualika kuperform pamoja kolabo zao kwenye Cotton Fest mwaka jana.

NB: Bifu zote AKA alizimaliza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live