Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Bidhaa za kushea nywele zenye kemikali kupigwa marufuku

Nywele Msa Bidhaa za kushea nywele zenye kemikali kupigwa marufuku

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka inayohusika na udhibiti wa Chakula na Dawa ya nchini Marekani (FDA), imesema inafikiria kupiga Marufuku bidhaa kadhaa zenye Kemikali ambazo hutumika kunyoosha nywele.

Kemikali hizo maarufu kwa jina la Kiingereza kama ”Relaxers” zimehusishwa na magonjwa kadhaa ikiwemo Saratani.

Kemikali hizo zinapokutana na joto hutoa gesi ijulikanayo kama ”formaldehyde”. Uvutaji wa hewa hiyo huweza kusababisha matatizo ya kiafya ikiwemo kuwashwa macho, koo, kikohozi, maumivu ya kifua, kuumwa kichwa mara kwa mara, pumu na saratani za tumbo na matiti.

Utafiti wa kitaalamu umebaini kuwa Wanawake wanaotumia kemikali hizo mara kwa mara wana hatari zaidi ya kupatwa na matatizo ya kiafya ikiwemo saratani za kizazi na hata ugumu wa kushika ujauzito.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live