Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Bibi wa miaka 60 kufunga ndoa na kijana wa miaka 27 Tabata

Bibi Tresss Bibi wa miaka 60 kufunga ndoa na kijana wa miaka 27 Tabata

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ule msemo wa Ng'ombe hazeeki maini umejidhihilisha kwa wanandoa watarajiwa ambao wamekuwa gumzo mitandaoni baada mpishano wa miaka yao kuzidi kiwango ambapo mwanamke "Bibi harusi" ana miaka 60 huku mwanaume "Bwana harusi" ana miaka 27 na kwa maana hiyo ni kwamba mke kamzidi mwanaume miaka 33.

Licha ya watu kutoa mitazamo tofauti-tofauti juu ya ndoa ya wawili hao,lakini kwa upande wao haijawa nongwa hata kidogo, hasa kwa bibi harusi ambaye ameahidi kumzalia mumewe pindi tu watakapofunga pingu za maisha hiyo siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Tabata Hotel.

Kijana anasema aliamua kumtongoza kikongwe huyo baada ya kuona dalili zote za bibi huyo kumtaka kimapenzi, kwani alikuwa anamchombeza kwa vijimaneno vya hapa na pale ikiwemo kumpikia kila siku bila nalipo na kumtoa out. Bibi harusi huyo ambaye mumewe wa awali alifariki miaka minne iliyopita amesema hajiwezi kwa Kijana huyo mwenye umri sawa na mjukuu wake.

Amesema anamiliki nyumba sita, ana gari na ana miradi yake inayomuingizia pesa, amesema hana shida ndogondogo ndiyo maana hata kwenye harusi yake hajachangisha mchango kwasababu anajiweza kiuchumi, kwa pesa zake mwenyewe ameandaa shughuli hiyo na kila atakayefika ukumbini hapo atakula na kusaza huku yeye mwenyewe akiwa ameandaa magauni matatu tofauti-tofauti atakayovaa kwenye harusi hiyo.

Amewataka wadada wa Mjini wanaomsumbua mume wake waache mara moja, kwasababu wamechelewa. Pia amewajibu walimwengu wanaosema anatumia pesa zake vibaya, amesema pesa alitafuta kwa jasho lake, wamuache atumie pesa zake kwasababu kama kusaidia wasiojiweza anawasaidia sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live