Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Bibi wa miaka 104 avunja rekodi ya kuruka angani

Dorothy Hoffner Dorothy Hoffner.

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dorothy Hoffner, bibi kizee mwenye umri wa miaka 104 kutoka Chicago nchini Marekani, ameweka rekodi ya dunia ya kuwa binadamu mzee zaidi kuwahi kuruka kutoka angani (sky diving), tukio lililotokea Jumapili ya Oktoba 1, 2023.

Kikongwe huyo amevunja rekodi ya Guiness World Record, iliyokuwa inashikiliwa na Linnéa Ingegärd Larsson wa Sweden ambaye aliiweka Mei, 2022 akiwa na umri wa miaka 103.

Hii ni mara ya pili kwa Dorothy kuruka kutoka angani ambapo mara ya kwanza alifanya akiwa na umri wa miaka 100. Tukio hilo lilianzia ndani ya ndege ya Kampuni ya Skyvane katika Mji wa Ottawa, Illinois katika Jimbo la Chicago.

Akiongozwa na mtaalamu wa mchezo wa kuruka kutoka angani (sky diving), Derek Baxter ambapo waliruka futi 13,500 kutoka usawa wa bahari na kutua salama ardhini wakitumia dakika saba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live