Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Bibi harusi afyatua risasi hewani na kutokomea kusikojulikana

Harusi 01 Bibi harusi qfyatua risasi

Mon, 10 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi katika jimbo la kaskazini mwa India la Uttar Pradesh wanamsaka mwanamke aliyefyatua bunduki kwenye harusi yake.

Video kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha mwanamke huyo akifyatua risasi nne hewani akiwa ameketi karibu na mumewe.

Polisi wa eneo hilo walisema wameandikisha kesi dhidi ya mwanamke huyo ambaye ametoweka tangu tukio hilo.

Milio ya risasi wakati wa harusi ni jambo la kawaida katika baadhi ya majimbo ya kaskazini mwa India na mara nyingi husababisha majeraha na hata vifo .

Kulingana na sheria za India, mtu yeyote anayetumia bunduki “kwa kwa kutowajibika au kwa uzembe au kusherehekea”, na kuwaweka wengine hatarini, anaweza kufungwa jela au faini au zote mbili.

Mnamo mwaka wa 2016, mahakama katika mji mkuu wa Uttar Pradesh, Lucknow, ilikuwa imeamuru kwamba kila tukio la kupigwa risasi kwa sherehe linapaswa kuchunguzwa bila kujali kama malalamiko ya polisi yalikuwa yamewasilishwa.

Kulingana na gazeti la Times of India, video ya bibi harusi ilirekodiwa na jamaa, ambaye pia aliiweka kwenye mitandao ya kijamii.

Polisi waliambia jarida hilo kuwa mwanamke huyo “anatoroka” kwa sababu aliogopa kukamatwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live