Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Bibi ahitimu kozi ya muziki TaSUBa

58641d12828ab4c650ce1153529b0a9e Bibi ahitimu kozi ya muziki TaSUBa

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mwanamke wa miaka 63, Joyce Kabadi ni miongoni mwa wanafunzi 58 waliohitimu kozi ya muziki katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).

Kabadi akihitimu Jumamosi, Machi 12, mwaka huu mafunzo ya muziki katika chuo cha TaSUBa, mkoani Pwani, akieleza na kudhihirisha kuwa, elimu haina mwisho.

Akizungumza na HabariLEO baada ya mahafali yao yaliyowahusu waamini 58 wa Kanisa la Waadventista Wasabato, Kabadi anayeishi Londo-Mbingu, Ifakara, mkoani Morogoro, alisema alianza kuimba zaidi ya miaka 20 iliyopita kanisani na akaona ili kipawa alichopewa na Mungu kiwe na maana, lazima apate ujuzi.

"Nimeanza kuimba muda mrefu na nitaimba maisha yangu yote nikiwa hai, sina mpango wa kuacha kuimba. Tusiogope uzee, tumtumikie Mungu bila kuchoka," alisema Kabadi.

Kabadi ana watoto tisa na wajukuu zaidi ya 25. Mbali na kuimba anajishughulisha na kilimo nyumbani kwake Ifakara mkoani Morogoro.

Kozi ya muziki aliyosoma Kabadi ni ya mwezi mmoja kuanzia Februari 14 hadi Machi 12, mwaka huu.

Mkuu wa TaSUBa, Dk Herbert Makoye alisema wahitimu 58 wa Kanisa la Waadventista Wasabato nchini wamehitimu mafunzo hayo ya muziki ikiwa ni muendelezo wa kanisa hilo kutumia chuo hicho kunoa vipawa vya waumini wao kuanzia mwaka 2018 walipoanza kupata mafunzo hayo chuoni hapo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz