Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bibi Cheka afariki dunia

86356 Bibipic.png Bibi Cheka afariki dunia

Fri, 29 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva, Cheka Hija maarufu Bibi Cheka amefariki dunia leo mchana Alhamisi Novemba 28, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila alikokuwa akipatiwa matibabu ya moyo.

Bibi Cheka alianza kufahamika katika tasnia ya muziki mwaka 2012 kupitia wimbo wa Ni Wewe alioimba pamoja na kundi la Wanaume TMK.

Alijizolea umaarufu kutokana na kuwa msanii mwenye umri mkubwa kuimba muziki wa kizazi kipya.

Akizungumza leo Adam Juma, mtoto wa Bibi Cheka amesema mama yake amefariki dunia saa 6 mchana. Amesema tangu Novemba 22, 2019 alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo.

“Mama alianza kuumwa muda lakini tulikuwa tukimuuguza nyumbani kwa kumnunulia dawa si unajua tena hali zetu, hata hivyo ilipofika Novemba 20 hali yake ilibadilika tukampeleka hospitali ya Mbweni.”

“Novemba 21 walituandikia twende Mwananyamala na ilipofika Novemba 22 tukapewa rufaa kwenda Hospitali ya Mloganzila,” amesema.

Juma amesema madaktari walijitahidi kuokoa maisha ya mama yake lakini ilishindikana. Bibi Cheka ameacha watoto wawili na wajukuu sita.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz