Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bi Hindu mgonjwa, Diamond, Simba SC wajitokeza kumsaidia

98689 Pic+hindu.png Bi Hindu mgonjwa, Diamond, Simba SC wajitokeza kumsaidia

Wed, 11 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Msanii Chuma Suleiman ‘Bi Hindu’ yupo kitandani akiugua kwa zaidi ya mwezi sasa tangu alipofanyiwa upasuaji wa kuondoa goita kwa mara ya pili.

Mjukuu wake Badra Hanya amesema Bi Hindu alifanyiwa upasuaji mwezi mmoja ulioisha, lakini goita ilirudi na kulazimika kufanyiwa nyingine wiki mbili zilizopita.

“Tangu alipofanyiwa hali yake haijawa nzuri kwani amekuwa akilalamika kupata maumivu ya mkono upande upande wa kulia.

“Kwa mujibu wa Daktari alituambia jambo hilo linaweza kuwa limechangiwa na goita ambalo huwa linatabia ya kutema sumu linapokuwa mwilini mwa mtu na kutuandikia dawa kwa ajili ya kupunguza maumivu huku akitutaka turudi mwisho wa mwezi huu wa tatu kuona maendeleo yake,” amesema Badra.

Mjukuu huyo amesema bibi yake analalamika kupata maumivu hadi kujikuta anakosa usingizi, wamepanga kwenda wiki ijayo kwa kuwa mwisho wa mwezi wanauona mbali.

Katika hatua nyingine, Diamond Diamond Platnumz tayari ameonyesha nia ya kumsaidia msanii huyo na meneja wake Babu Tale ameshakwenda kumuona Bi Hindu jana Jumanne.

Pia Soma

Advertisement
Juzi Diamond baada ya kuona kipande cha video kikionyesha kuumwa kwa bibi huyo, aliaandika”Babu Tale lishughulikie’.

Mwananchi ilitaka kujua kama tayari wameshawasiliana na uongozi wa msanii huyo, ambapo Badra amesema washawasiliana kwani juzi Tale alimpigia simu na jana alifika nyumbani kumuona na kuzungumza nao mambo mbalimbali ambayo hakuwa tayari kuweka wazi.

Wakati kuhusu kituo cha redio ambacho bibi huyo anafanya kazi kama mtangazaji kwa sasa, amesema kimekuwa msaada kwao tangu operehseni ya kwanza hadi sasa.

Wakati timu ya Simba ambapo bibi huyo ni moja ya wahamasishaji wakubwa na mwanachama wa timu hiyo, amesema tayari walishatuma msaada wao na bado wanaendelea.

Badra amesema kwa kuwa bibi huyo bado anaumwa ameomba wadau mbalimbali wakiwemo mashabiki wake kushirikiana na familia katika kumuhudumia kwa kuwa peke yao hawataweza ukizingatia anamahitaji mengi kwa sasa.

Chanzo: mwananchi.co.tz