Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beyonce aongoza uteuzi tuzo za Grammy

Beyonce Beyonce aongoza uteuzi tuzo za Grammy

Wed, 16 Nov 2022 Chanzo: Voa

Tangazo la walioteuliwa kuwania tuzo za Grammy mwaka huu limetolewa Jumanne Novemba 15, na linaonekana kuwaweka tena katika jukwaa kwa ushindani kati ya waimbaji Adele na Beyonce kuwania tena nafasi ya juu, katika sehemu mbili tofauti za mashindano hayo kama ilivyokuwa hapo mwaka 2017.

Muimbaji mashuhuri wa Marekani, Beyonce, anaongoza katika orodha ya wateule wa nishani za Grammys, akipata teuzi 9 za dhahabu, akiwa anaongoza, na Kendric Lamar, akiapta teuzi 8 nae muimbaji Adele kutoka Uingereza akipata teuzi 7 kadhalika muimbaji Brandi Carlile, ambaye nae pia amepata teuzi 7.

Tangazo la wateuzi wa mwaka huu wa Grammys limetolewa Nov 15, 2022, na linaonekana kuweka tena stegi, waimbaji Adele na Beyonce kunangania tena nafasi ya juu, katika sehemu mbili tofauti za mashindano hayo kama ilivyokuwa hapo mwaka 2017.

Baadhi ya wale waloteuliwa kunangania tuzo la albumu ya mwaka ni pamoja na Kendric Lamar, Adele, Brandi Carlile, Lizzo, Bad Bunny, Mary J Blige, HarryStyles, Abba, Coldplay na Beyonce. Utambuzi na uteule wa Beyonce unafwatia kutowa kwa albamu yake kabambe yenye miondoko ya disco ijulikanalo kama "Renaissance".

Albamu iitwayo "Mr. Morale And The Big Steppers", la Kendik Lamar, Adele nae na albamu yake 30 nae Brandi Carlile na albamu yake, In These Silent Days.

Waimbaji hawa wanne kadhalika nyimbo zao zimeteuliwa katika kundi la rekodi ya mwaka. Wimbo wa Adele, Easy On Me, ulitia fora sana hapo mwaka jana.

Chanzo: Voa