Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beyoncé na Swift wang’ara onyesho la kwanza la filamu la Renaissance

Beyonce . Beyoncé na Swift wang’ara onyesho la kwanza la filamu la Renaissance

Fri, 1 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Beyoncé aliwaambia mashabiki wanapaswa "kudensi, kuimba, kucheka na kulia" walipokuwa wakitazama onyesho la kwanza la London la filamu yake ya ziara ya Renaissance.

Akiwa amevalia suti nyeupe, nyota huyo alijitokeza kwa muda mfupi mbele ya fonyesho hilo liliyodumu kwa saa tatu, na kuwaambia watazamaji "wajisikie huru".

Taylor Swift, ambaye filamu yake ya tamasha ilivunja rekodi mapema mwaka huu, pia alikuwepo.

Binti yake Beyoncé Blue Ivy pia alihudhuria hafla hiyo.

Wageni wengine ni pamoja na nyota wa Destiny's Child Michelle Williams, mwanamuziki will.i,am, mhariri wa zamani wa jarida la mitindo Vogue Edward Enniful, na muigizaji Vivica A. Fox.

Wote walivaa "vazi rasmi la kifahari" waliloomba kulivaa kwa ajili ya tukio hilo.

Muonekano wa Swift ulikuja baada ya Beyoncé kuhudhuria onyesho lake la kwanza la tamasha la Hollywood lililoitwa Eras Tour y tarehe 11 Oktoba.

Chanzo: Bbc