Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beyoncé adaiwa kuwa chanzo cha mfumuko wa bei Uswidi

Beyonce Adaiwa Kuwa Chanzo Cha Mfumuko Wa Bei Uswidi Beyoncé adaiwa kuwa chanzo cha mfumuko wa bei Uswidi

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Je, ulifikiri kuwa vita vya Ukraine au misururu ya ugavi ndio chanzo cha kupanda kwa bei za bidhaa? Nina hakika kuna kitu usichokijua kuhusu Beyoncé.

Kuanza kwa ziara ya dunia ya mwimbaji huyo nchini Uswidi mwezi uliopita kulizua mtafaruku mkubwa wa mahitaji ya hoteli na migahawa ambayo imeonekana katika takwimu za uchumi wa nchi hiyo.

Uswidi iliripoti mfumuko wa bei wa juu-kuliko ilivyotarajiwa wa 9.7% mwezi Mei.

Kupanda kwa bei za hoteli na mikahawa kulisababisha mshangao huo.

Michael Grahn, mwanauchumi katika Benki ya Danske, alisema alifikiri Beyoncé alichangia kupanda kwa gharama za hoteli.

Anaweza pia kuwa ndiye aliyesababisha ongezeko kubwa lisilotarajiwa la bei za burudani na bidhaa za utamaduni, alisema.

"Singemlaumu Beyoncé kwa mfumuko wa bei wa juu, lakini maonyesho yake na mahitaji ya kimataifa ya kumuona akiigiza nchini Uswidi yalionekana kuwa yameongeza kidogo," aliandika katika barua pepe kwa BBC.

Kuna shaka kidogo kwamba ziara ya kwanza ya mwimbaji huyo katika miaka saba inaashiria nyakati kubwa kiuchumi.

Angalau moja ya makadirio yanapendekeza kunaweza kuingiza karibu £2bn kufikia mwisho wake mnamo Septemba.

Utafutaji wa malazi katika miji kwenye ziara uliongezeka baada ya kutangazwa kwa ziara yake, Airbnb iliripoti.

Tikiti za tamasha nyingi ziliuzwa ndani ya siku chache na bei zilipanda kwenye soko la mauzo.

Nchini Uingereza, watu 60,000 walifika Cardiff, wakiwemo mashabiki kutoka Lebanon, Marekani na Australia.

Hitaji la vyumba vya hoteli vilivyounganishwa kwenye tamasha lake huko London lilikuwa kubwa sana hivi kwamba katika kisa kimoja, baadhi ya familia zisizo na makazi zilizowekwa katika hoteli na halmashauri ya eneo hilo ziliripotiwa kulazimishwa kutoa nafasi kwa mashabiki wake.

Tamasha za Stockholm, ambapo Beyoncé alicheza na umati wa watu 46,000 kwa siku mbili za usiku, zimeripotiwa kuwavutia mashabiki kutoka kote ulimwenguni - haswa Marekani.

Katika barua pepe kwa Washington Post mwezi uliopita, ‘Visit Stockholm’ ilielezea kukua kwa utalii katika jiji hilo kama "matokeo ya Beyoncé" .

Mfumuko wa bei nchini Uswidi ulifikia asilimia 12.3 mwezi Desemba.

Kiwango cha 9.7% mwezi uliopita kilipungua kutoka 10.5% mwezi wa Aprili, takwimu rasmi zinaonyesha. Masoko ya fedha yalitarajia karibu 9.4%.

Kwa nyota mmoja kusababisha matokeo kama hiyo "ni nadra sana", Bw Grahn aliambia BBC, akiongeza kuwa mashindano makubwa ya kandanda yanaweza kuwa na matokeo sawa.

Aliandika kwenye mitandao ya kijamii kwamba alitarajia mitindo kurejea katika hali ya kawaida mwezi Juni.

Chanzo: Bbc