Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bendera ya Cameroon jukwaani yamponza Libianca

LIbianca Faces Death Threats Scaled Libianca

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Libianca ni Msanii kutokea nchini Cameroon aliyetambulishwa vyema Na Wimbo wake Wa people.

Siku Tatu Nyuma ameweka open letter akielezea kupokea vitisho Vya kuuawa Kutoka kundi La "The Amba Boys" Ambalo halikubaliani Na Utawala uliopo Wa Rais Paul Biya

Vitisho Hivyo vimekuja Mara Baada ya kunyanyua bendera ya Cameroon Alipokuwa Anafanya Tamasha lake Huko Australia, Na kitendo Hiko kimeonekana Kama Anam support Rais Biya.

Libianca Ameamua Kusitisha Ziara yake ya kimziki aliyokuwa anatarajia kuifanya Huko North America.

Ndani ya barua Hiyo ameelezea Kuhusu civil war inayoendelea Toka 2016 Ambayo imepelekea Vifo visivyo Na Idadi Vya Watu wake Lakini Pia Watu wakitengana

Ameendelea kusema Kuwa kunyanyua kwake bendera Haikuwa kuonyesha Upande aliopo bali kuonyesha Iman Kuwa Inakuwa vizuri wakisimama Pamoja Kuliko kuchukiana, Bendera Sio ya Paul Biya, Bendera ni Kwa Ajili ya wananchi

Barua Hiyo Kwa Tafsiri Isiyo Rasmi Hii hapa

Mwaka uliopita nashukuru niliishi kutimiza Ndoto Zangu Za Toka Nikiwa Mdogo, kuifanya familia Yangu, Sehemu nikiyotoka Na Nchi Yangu kujivunia, Na Hilo limeondolewa Na Watu Ambao wameamua kuchagua Upande Katika matatizo yanayoendelea, niliamua kukaa Kimya Kwa Sababu Siku Zote Upande niliouchagua ni kusimama Na Watu Wangu.

Mimi Sio mwanasiasa, ni raia Wa Kawaida Tu Ambaye Nataka amani Na upatanisho. Familia Yangu, Kanisa Langu, wafanyakazi Wangu Na Marafiki Zangu wameathiriwa Sana Na vitisho Hivi, Lakini pia vimeharibu Mipango Yangu ya Kurudi Cameroon kusheherekea mafanikio Yangu Na Watu wangu. Sitavipa Nafasi vitisho, nimeamua kuyatangaza Mazuri ya Cameroon Na vipaji Vya Watu wake, Na sitaruhusu Mtu Yoyote aniondolee Hilo.

Ni Ukweli mchungu kumeza, Lakini najali Zaidi Mbali Na usalama Wangu Binafsi, Nafikiria Kuhusu Kaka Na dada Zangu, mama Na baba Zangu, Ambao wanahitaji amani Na utulivu, Lakini Wanaishi Katika Hii vita. Nawaombea Wote waliopoteza uhai, Lakini pia wanaombea Wote Ambao wanaendelea kuteseka Kutokana Na vita Hii. Sisi ni Bora Kuliko haya.. Huu Ni Ujumbe Wangu Kwa serikali Na separatist movement of Cameroon "WAACHENI WATU WANGU"

Tarehe Mpya Za tour Yangu ya north America zitatangazwa zitakapoamuliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live