Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ben Pol ayamaliza na Jux

Ben Pol Jux Mas Ben Pol ayamaliza na Jux

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Staa wa Muziki wa R&B @iambenpol siku ya jana kulalamika kuwekwa kwenye orodha ya Mastaa watakaokuwepo kwenye uzinduzi wa album ya @juma_jux, mambo yalibadilika baada ya Ben kumkataa msanii huyo.

Ben Pol alifunguka na kusema kuwa hajaalikwa na wala hakuna makubaliano yoyote, kati ya management ya wasanii hao kuhusu kuhudhuria uzinduzi wa albam hiyo ya #KingOfHearts.

Imefahamika kuwa, hatimaye mastaa hao wameyamaliza na kuelewana, hivyo sasa Ben Pol atakuwepo siku ya leo kwenye uzinduzi huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram wa #BenPol ameandika; "Barabara zote kuelekea #TheSuperDome #Masaki leo. It’s @juma_jux #KingofHearts Day! Asante kwa kikao chetu cha leo #MoreLoveLessEgo ❤️ We gon turn up TONIGHT! #PartyModeOn."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live