Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ben Pol ataenzi haya kwa Hayati Magufuli

Pic Ben Pol Data.png Ben Pol ataenzi haya kwa Hayati Magufuli

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MSANII wa Bongo Fleva, Ben Pol amesema Tanzania imepata pigo kubwa la kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli ambaye aliamini katika kuchapa kazi kuwa msingi wa maendeleo.

Ameliambia Mwanaspoti Online, leo Jumamosi ya Machi 20,2021 kwamba kutokana na alama ya uchapakazi aliyoiacha itakuwa nguzo ya kujituma na kufanya kazi kwa bidii, ili kufikia malengo ya Tanzania yenye nguvu kwa kila sekta, itakayokuwa inaigwa na mataifa mengine.

" Kaondoka shujaa, mchapakazi, aliyejituma kusisitiza kufanya kazi kwa vitendo, lakini hatuna budi kumshukuru Mungu katika nyakati zote, maana yeye ndiye anatoa zawadi ya pumzi ya mtu na ndiye mwamuzi wa mwisho kuichukua," amesema na ameongeza kuwa;

"Jambo la msingi tunapaswa kumuenzi kwa matendo yale ambayo alitamani yafanyike katika nchi yetu na kumuombea aliyechukua majukumu yake kwamba Mungu ampe nguvu na hekma ya kuongoza Watanzania wenye matumaini makubwa na yeye,"amesema.

Amesema kwa upande wake atamkumbuka katika mambo mengi hasa kuwatia moyo vijana waliokuwa wanaonyesha bidii katika kazi yao na kwamba ameacha matendo yanayoishi ambayo hayatasahaurika.

"Hakuna kitu kizuri ukiondoka duniani ukiacha vitu vinavyoishi ambavyo watu watakuwa wanataja jina lako kila wanapoviona, hii inatufunza tuliobaki kwamba dunianiĀ  tunapita tunapaswa kuishi kwa kutenda mema na sio mabaya yatakayotunyima pumziko la amani," amesema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz