Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ben Pol anavyojipanga kutoa nyimbo kali 2024

Pic Ben Pol Data.png Ben Pol anavyojipanga kutoa nyimbo kali 2024

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol amesema mwaka huu utakuwa wa kutoa nyimbo bandika bandua, zitakazokuwa zinaishi kwa mashabiki wa muziki wake na anachokizingatia kwenye utunzi ni uhalisia ulivyo kwenye jamii.

Miezi mitatu nyuma, alitoa wimbo wa 'My Life', aliomshirikisha mwana Hip Hop, Darasa na ulifanya vizuri na sasa kaachia mwingine unaokwenda kwa jina la I'm in Love, alioimba na Phina.

"Nimeona mapokeo ni mazuri, yananipa picha ya kazi gani wanazihitaji zaidi, wimbo wa My Life nilioimba na Darasa ndani yake uneelezea hakuna kitu kipya kwenye dunia, inabidi maisha mengine yaendelee bila kujali mazingira gani mtu anapitia," amesema na kuongeza;

"Kila msanii ana aina yake ya uimbaji ambayo mashabiki wake wanaipenda, hivyo wajiandae kusikiliza nyimbo nzuri za kuwajenga na kuwaburudisha."

Ben Pol amewahi kutamba na nyimbo mbalimbali kama Moyo Mashine, Wapo, Nyumbani, maneno na nyingine nyingi.

Chanzo: Mwanaspoti