Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Ben Pol ametoa povu kuhusu kitendo cha Msanii mwenzie wa Bongo Fleva, Jux kuchapisha mabango mtandaoni kuwa atakuwepo katika uzinduzi wa albamu yake ya ‘King of Hearts’ utakaofanyika Desemba 7 mwaka huu, kwa madai hakuna makubaliano yoyote kati yao.
"Una namba yangu umeshindwa kunipigia au kunitumia ujumbe? au watu wako kuwasiliana na watu wangu? Tunakuja kuona kwenye mitandao kwamba nitakuwepo kwenye show yako.
"Wewe ulikasirika kwa Harmonize kukuweka kwenye matangazo ya event yake bila kukutaarifu au kukualika, ukafanya hadi interviews lakini na wewe unafanya kitu kilele. Napenda sapoti lakini hii ni style gani kaka," ameandika Ben Pol kwenye mitandao.