Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ben Pol, Anerlisa ndani ya Kidani

14c9f47fbc29c2aa9d710d8ea6514f9f Ben Pol, Anerlisa ndani ya Kidani

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Behnam Paul, ‘Ben Pol’ ameachia video ya wimbo wake mpya wa Kidani ambao amemshirikisha mke wake mtarajiwa Anerlisa kama video vixen.

Wimbo huo umeachiwa juzi na Ben Pol na alisema video hiyo imefanyika Dar es Salaam.

"Video hii inaweza kuwa ni uthibitisho kuwa ndoa yangu na Anerlisa bado iko imara pia naendelea kutoa shukrani za dhati kwa wapenzi wangu kwa ushirikiano wanaonipa na nimeona niandae burudani kwao," alisema Ben Pol.

Alisema kuwa ameandaa usiku maalumu Desemba 31 utakaofanyika Ramada Hotel ili kutoa burudani kwa mashabiki wake.

Ben Pol alisema kuwa siku hiyo atashusha burudani ya kufunga mwaka na amewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi ili kuanza mwaka kwa pamoja.

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa ya kuvunjika kwa ndoa ya Ben Pol na mkewe Anerlisa na sintofahamu hiyo ilizidi kushika kasi baada ya msanii huyo kubadili dini na kuingia katika Uislamu.

Chanzo: habarileo.co.tz