Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Belle 9: Hip Hop ni kama Serikali

Belle 9 Jkm Belle 9: Hip Hop ni kama Serikali

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfalme wa RnB Bongo 'Belle 9' auhusisha muziki wa Hip-hop na utawala wa Serikali kutokana na wanamuziki wa miondoko hiyo kuwa na wigo mpana wakuijua jamii inayowazunguka.

Mkali huyo wa ngoma ya "Marafiki" amepigia mstari kupitia "The Splash" ya "Ebony FM", kutokana na aina ya maisha yake ndani na nje ya Muziki kuwa na Urafiki mkubwa na wanamuziki wa Hip-hop.

"Aaah kuwa na ukaribu na Wasanii wa Hip-hop hiyo ni just a nature imetokea tu sio kitu ambacho nimewahi kuki-plan lakini ni watu ambao unakuta ile heshima ambayo wananipa kwanza ndio kitu ambacho labda kinatengeneza tuwe marafiki.

"Yaani watu wa Hip-hop wanakuwaga kama vile ni Serikali yaani unaweza ukafanya Chorus ya mtu Fulani ukashangaa jamii yake kwa ukubwa sana inakuheshimu au inakupa ile thamani yako nadhani ndio hicho kitu," amepepeta maneno Belle.

"Tunaongea lugha moja ni watu ambao wanajifunza mambo mengi, yaani ni watu ambao wanapenda Kujifunza mambo mengi, yaani ukikutana na msanii wa Hip-hop ambae hajui mambo mengi ni wachache sana kwa hiyo Mimi pia huwa najifunza kwa sababu huwa napenda kujua vitu zaidi ya ambavyo na vijua," amesisitiza zaidi 'Belle 9'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live