Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Belle 9, Bonge la Nyau, Lulu Diva watoka hospitali

Pc 0 Belle 9, Bonge la Nyau, Lulu Diva watoka hospitali

Wed, 9 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WASANII, Abednego Damian ‘Belle 9’, Lameck Jacob ‘Bonge la Nyau’ na Lulu Diva, wameruhusiwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jana baada ya kuonekana hali zao hazina tatizo.

Wasanii wao walipata ajali maeneo ya Mwidu, Chalinze wakielekea Dar es Salaam wakitoka kwenye kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Iringa, ambapo awali walilazwa Kituo cha Afya Chalinze, Pwani na juzi wakahamishiwa Muhimbili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankiyo Nyigesa, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema gari aina ya Toyota IST waliyokuwa wamepanda wasanii hao iliacha njia na kupinduka na kwamba walipata michubuko midogo mwilini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Msaidizi wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa hospitali hiyo, Sophia Mtakasimba, alisema waliwapokea wasanii hao juzi saa 8:30 mchana na kuchukuliwa vipimo kwa ajili ya uchunguzi.

“Ni kweli tuliwapokea wasanii hao, wakafanyia vipimo wawili, Bonge la Nyau na Bele 9 hawakulazwa, lakini Lulu Diva alilazwa na leo (jana) ameruhusiwa,” alisema Sophia.

“Mwenyezi Mungu ametunusuru kwenye ajali mbaya iliyotokea tukiwa njiani maeneo ya Chalinze,” alisema Bongo la Nyau.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, aliwashukuru watu wote waliowasaidia wasanii hao tangu walipopata ajali hadi kuruhusiwa kutoka hosptali.

Chanzo: habarileo.co.tz