Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bella: Sina dini, ni biashara za wazungu hizo

Bella Srtsss Bella

Wed, 10 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa mrembo wa Mkoa wa Ruvuma na msanii wa Bongo Movies, Isabela Mpanda 'Miss Bella' amesema kuwa yeye hana dini kwani dini zote zililetwa na Wazungu kibiashara na kama kivuli cha ukoloni.

Bella amesema hayo wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari huku akidai kuwa iwapo dini zingekuwa na nia moja basi Wakristo wangekuwa wakisali kanisa moja na Waislam wote msikiti mmoja.

"Mimi siyo Mkristo wala siyo Muislam, siwezi kuwa kwenye hizo dini maana ni za wazungu, wazungu walituletea dini zao wakazigeuza kwa kivuli cha kumtumikia Mungu wakati hizo dini zimeletwa kibiashara.

"Ndio!!! zipo kibiashara wala hakuna dini ya kweli hata moja hapo, kama ingekuwa dini ya kweli basi wote tungesali kanisa moja, kama ni Wakristo wangesali kanisa moja kwa umoja na Waislamu wangeswali Msikiti mmoja kwa umoja.

"Leo hii makanisa yamekuwa mengi kushinda nyumba za watu, siyo dini tena imekuwa biashara, mimi nina baa yangu nauza pombe, lakini wateja wangu wengi ni Wachungaji.

"Yaani mtu anakopa pombe halafu anakwambia nitakulipa Jumapili nikipata sadaka, Waafrika nao wamekuwa kama wajinga, mtu anahangaika wiki nzima kutafuta pesa akipata anaenda kumpa Mchungaji pesa zote siku ya Jumapili halafu anaanza upya kutafuta.

"Hata kwa Waislamu nao ni hivyo hivyo, wamegawanyika wapo Waislamu aina mbili, yote hiyo ni kwa sababu ya kibiashara watu wana tamaa ndiyo maana wanaona Misikiti iwe mingi, mimi sina dini mimi ni "Mwana jadi" yani sisi Wana jadi tunaishi maisha yetu ya asili na tunamtukuza "Mungu mwenye vyote".

"Hii dini ndiyo dini yetu ya asili ambayo wote tunatakiwa tuifuate tuachane na hizi dini za Wazungu.

"Yaani Wazungu haohao waliotuletea dini, leo haohao ndiyo wametuletea Ushoga na Usagaji, sasa kama wana hofu ya Mungu kwanini watuletee haya mambo, mimi kama mama naumia sana, nawahurumia Waafrika ambao mpaka leo bado wanawasujudia wazungu kwa kuabudu dini zao.

"Watu wanaacha kuwaabudu Wazee wao waliotangulia mbele za haki wanawaabudu Wazee wa kizungu ambao wanaitwa (Mtakatifu Anthony) sijui Mtakatifu nani huko hao ni Wazee wa kizungu waliofariki.

"Mimi na Mume wangu tumefunga ndoa ya Jadi, hiyo ndoa haijafungwa Kanisani, Msikitini wala Mahakamani, ni ndoa ya kijadi ambayo tumefungishwa na wazee na inatambulika na Mungu mwenye vyote," amesema Miss Bella.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live