Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beka Flavour awaumbua mashabiki mitandaoni

BEKA Beka Flavour awaumbua mashabiki mitandaoni

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Beka Flavour amewaumbua baadhi ya mashabiki wa mitandao ya kijamii akisema asilimia 99 wanaitumia mitandao hiyo vibaya.

Member huyo wa zamani wa Yamoto Band amefunguka hilo kupitia #eNewz ya #EastAfricaTV zaidi msikie;

“Wanasema Tanzania ndiyo nchi inaongoza kwa matumizi ya mitandao, kwa hiyo hata hao waliotengeneza TiTok, Instagram na mitandao mingine ni kama waliitengeneza Tanzania na watu wanajua kuvitumia, siwalaumu.

“Kama mtu labda msanii ukibishana kuhusu mambo mabaya mtu ataweka bando au atakopa ili akaangalie. Ukiweka kitu kizuri watu wala hawahangaiki na wewe, kwa hiyo watu wanaitumia mitandao ya kijamii kwa ubaya kwa asilimia 99.

“Mtu akitoa ngoma katikati ya bifu la mtu na mtu wanabishana, unaona ngoma haifanyi vizuri, waaachana na muziki. Ni vitu ambavyo wamevimeza na vimeingia kwenye damu zao.

“Wapo wasanii wanafanya hivyo kama figisu tu kukutoa kwenye reli, anaona kabisa umeachia ngoma lakini anajaribu kutifuana na msanii mwenzake ili upepo uhame na ngoma yako isizungumziwe kabisa, lakini kama una ngoma kali, hata kama wakifanya je, ngoma itatikisa tu,” amesema Bekka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live