Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beka Flavour: Utimu unachangia kuua muziki

BEKA FLAVOUL Beka Flavour.

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji wa Bongofleva, Beka Flavour amesema hawezi kuruhusu masuala ya utimu yanayoendelea katika tasnia kuendesha na kuamua hatima ya muziki wake, kwani anaamini kazi nzuri itafanikiwa bila kuhusishwa na mambo hayo.

Beka Flavour alikuzwa kimuziki na kituo cha Mkubwa na Wanawe chake Mkubwa Fella, ni miongoni mwa wasanii waliounda kundi la Yamoto Band na wenzake watatu, Aslay, Enock Bella na Mbosso aliyekuja kusainiwa na WCB Wasafi.

Baada ya kuvunjika kundi la Yamoto Band alianza kufanya kazi kama solo ambapo wimbo wake ‘Libebe’ (2017) ndio ulimtambulisha na kufuatiwa na nyingine zilizofanya vizuri kama 'Kibenten', 'Poa Poa', 'Sarafina', 'Naona Kiza' n.k.

Akizungumza na gazeti hili, Beka Flavour amesema siku zote amekuwa anafanya muziki mzuri kwa ajili ya mashabiki wake ambao wapo naye kwa ajili ya ubora wa kazi zake, na sio timu ambazo kamwe hawezi kujiunga nazo.

"Kweli utimu unachangia kuua muziki ila kwenye hilo siwezi kusema sana kwa sababu sina timu, yaani mimi mwenyewe sina timu yangu, yaani timu Beka. Hivyo sitoruhusu kuwa kwenye timu ya aina yoyote, mtu ambaye anapenda muziki wangu, atanisapoti, mtu ambaye anasapoti kwa ajili ya muziki wa timu hiyo basi awe nao tu.

"Naimba muziki mzuri ambao kila mtu ataupenda, lakini hao wenye timu zao kuna vitu vinawafaidisha, kama vina manufaa, basi waendelee kuvifanya ila kwa upande chanya, wasifanye kwa mambo mabaya kwa sababu zikizidi sana watu wanaweza kuumizana," alisema Beka.

Tangu aingie kwenye muziki, Beka Flavour amefanikiwa kutoa albamu moja, ‘First Born’ (2022) yenye nyimbo 15, ambapo aliwashirikisha wasanii kama  Barnaba, Linah, Aslay, Enock Bella, Naiboi, Humble Smith na Christian Bella.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live