Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei za kutumbuiza Diamond, Davido, Burna Boy zatajwa, Tazama hapa!

Diamond Wizkid Burna Boy Davido Diamond, Davido, Burna Boy

Tue, 30 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fahamu kwamba, kwa mujibu wa chapisho toka gazeti la Nation Africa la nchini Kenya, limetaja bei ambazo wasanii Diamond Platnumz, Davido na Burna Boy wanalipwa kutumbuiza kwenye maonesho ya Kimataifa.

Kwa upande wa Diamond Platnumz, wameandika kwamba kwa sasa analipwa kiasi cha ($100,000) zaidi ya Tsh milioni 234 pia waandaaji wakilazimika kumgharamia usafiri wa ndege binafsi.

Vile vile waandaaji wanatakiwa kuhudumia vinywaji ikiwemo Whiskey chupa 12 za Bia, chupa 24 za maji muda wowote, taulo 12 za usoni na mengine.

Burna Boy yeye ametajwa kutoza kiasi cha ($500,000) zaidi ya Tsh Bilioni 1.1 kwa onesho moja la Kimataifa.

Pia waandaaji watalazimika kumuandalia ndege binafsi yenye kubeba watu 13, magari 8, basi pamoja na gari la kuwapokea wakiwasili. Vyumba 10 vya kulala vyenye ubora pia eneo la kuvuta (smoking).

Chumba chake kinatakiwa kuwa na vinywaji Hennessy, Jack Daniels na Champagne.

Kwa upande wa Davido, yeye alitoza kiasi cha ($300,000) zaidi ya Tsh milioni 700 kutumbuiza kwenye onesho moja nchini Kenya, japo waandaaji hawakulipa na kuahirishwa onesho hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live