Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bei ya nguo za Lulu zawatoa povu mashabiki

38172 Lulupic Bei ya nguo za Lulu zawatoa povu mashabiki

Thu, 24 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewatoa povu mashabiki wake baada ya kuanza kunadi bei za nguo zake alizotangaza kuanza kuziuza hivi karibuni.

Mwigizaji huyo aliyetamba na kundi la sanaa la Kaole akiwa binti mdogo, juzi Januari 22, 2019 alitangaza kuuza baadhi ya nguo zake na fedha itakayopatikana itakwenda kuwasaidia wasiojiweza ingawa hakuainisha kundi lolote.

Alianza kunadi nguo zake kupitia mtandao wa Instagram huku akiweka na bei ya kila nguo hali iliyoonyesha kupokelewa tofauti na mashabiki wake.

Baadhi walihoji bei hizo kuendana na uhalisi wa maisha hasa katika mwezi huu ambao kila mtu analalamika kuwa hana fedha kutokana na mfululizo wa sikukuu na majukumu ya mwanzo wa mwaka kama vile ada.

Wengine walihoji bei alizotaja iwapo zinaendana na thamani hali ya nguo zenyewe.

 “Yaani nusu ada ya mtoto nikanunue gauni ya kitambaa cha satini? huyo fundi aliyeshona yuko mbinguni au? Awe na huruma,” amehoji shabiki yake mmoja kuhusu gauni fupi la kijani alilotangaza kuliuza kwa Sh500,000.

Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Muu Msambaa amesema kwa gharama hizo anaweza kununua vitambaa na kushona nguo nyingi kadri anavyopenda.

Ingawa wengi walionekana kushtushwa na bei hizo lakini wengine walimtetea wakisema wenye uwezo watanunua na wasio nao wakae kimya.

“Nyie mnalalama wakati nguo ya laki nne imeshanunuliwa... tupambanae tu hali zetu. Sema sina sio hatuna.” 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz